WADAU asanteni sana kwa ushauri wenu, nimefika kituo kikuu cha Polisi mkoa wa Mbeya (Cetral) nikiwa nimeambatana na Mwandishi mwenzangu Ezekiel Kamanga majira ya saa tano na dakika 9 mpaka saa tano na dakika 25. Tulipoingia ndani ya kituo hicho tukaelekea moja kwa moja ghorofani ilipo ofisi ya Ofisa upelelezi wa wilaya ya Mbeya OC-CID Mtatilo ambapo hatujafanikiwa kumkuta. Baada ya kutoka katika ofisi hiyo tulielekea ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya hiyo OCD Silvester Ibrahim naye hatujamkuta na nilipojaribu kumhoji katibu muhtasi wake alisema kuwa viongozi wote hao walikuwa kwenye kikao katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya eneo la Mahakama kuu (FOREST MBEYA)! Tulipoomba kitabu cha wageni ili tusaini kuthibitisha kuwa niliitikia wito wao (Serikali) amekataa na kudai kuwa ni vema nikawapigia simu.... bila kufafanua kuwa gharama za simu zitakuwa juu ya nani. Baada ya hapo nimetoka na kumwandikia OC-CID huyo ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya kiganjani kuwa nilifika lakini sikubahatika kumkuta ofisini kwake. Ninachoweza kusema ni kwamba yawezekana kuna kazi zangu ziliwagusa kwa namna moja ama nyingine hasa zile zinazoonekana magazetini na katika mtandao wa kijamii ninaoumiliki na kuusimamia wa www.kalulunga.blgspot.com ambao umekuwa chanzo cha habari katika ofisi ya RPC tangu yupo kamanda Nyombi. Mbali na jambo hilo, miaka miwili iliyopita chini ya OCD huyu huyu waliwahi kunihoji kwa masaa mawili baada ya kutoboa jipu kwa wakuu wao mbele ya aliyekuwa msemaji wa polisi Abdallah Msika kwa wakati huo na kuweka wazi namba za majalada ya kesi ambazo zilikuwa zinatengeneza ulaji kwa baadhi ya wasaidizi wao nk....hali ambayo waliichukia sana... Hivyo nahisi kuwa yawezekana wamepata (ka-jambo) ka kuanzia na walitaka nifike saa moja asubuhi ili wanipeleke moja kwa moja kwa RPC wa mkoa wa Mbeya Diwan Athuman. Lakini yote na yote tunawaachia wenyewe na Mungu ataendelea kusimama upande wa haki, hata nikifa mimi ukweli ninaoufichua na kuiachia jamii itoe hukumu hautakufa. Ninasubiri zaidi maelekezo yao.....DAIMA MBELE, UKWELI DAIMA, TUMWABUDU MUNGU NA KUWATUMIKIA WATU KWA HAKI. REGARDS, Pastor Gordon Kalulunga, P.O.BOX 705, 0754 440749, 0655 440749 MBEYA-TANZANIA |
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
This years motto: 'WALK THE TALK'
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en