John Shabani na kundi lake wakilishambulia jukwaa.

John Shabani akiimba kwa hisia.
Mzee Cosmas Chidumule na Stara Thomas nao walikuwepo.
John Shabani (kushoto) akiwa na Bishop John Komanya (katikati) na Upendo Kilahiro (kulia) wakati wa tamasha hilo.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria tamasha hilo.
John Shabani akimsindikiza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh Fenella Mukangara.
Tarehe 10.06.2012, imebaki kuwa siku ya historia kwa maelfu ya wakazi
wa jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla. Ni lile tamasha la
kusifu na kuabudu pamoja na maombi maalum kwa ajili ya nchi ya Tanzania,
ambalo liliandaliwa na mtumishi wa Mungu, John Shabani.Katika tamasha hilo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh Fenella Mukangara. Mh Mukangara baada ya kuzindua DVD na BLOG ya John Shabani, pia aliongoza harambee ya kuchangia huduma ya mtumishi. KWA HISANI YA JOHNSHABANI