Tuesday, June 12, 2012

BOB MAKANI AAGWA DAR

Gari lililobeba mwili wa Bob Makani likiwasili mahali hapo.

Jeneza lililobeba mwili wa Bob Makani likiwasili.

Rais Kikwete akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Bob Makani.

Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) na mkewe mama Salma Kikwete wakiwasili mahali hapo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal naye akiwasili eneo hilo.

Rais Kikwete (katikati) akitaniana na viongozi wakuu wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Dr. Slaa.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiteta jambo na Katibu wa chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (katikati).

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kulia) akisalimiana na January Makamba.

January Makamba (kushoto), Freeman Mbowe (katikati) na Dr. Slaa. wakibadilishana mawazo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, leo aliungana na Watanzania wengine kuuaga mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mohamed Bob Makani katika Viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam aliyefariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Agha Khan.

Viongozi wengine wa Serikali waliokuwepo ni Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad. Pia alikuwepo mama Anna Mkapa na mama Salma Kikwete.

(PICHA ZOTE: ISSA MNALLY/GPL)