Dr. Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa: Serikali inawajibika kutueleza
by zittokabweUjumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI'Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous'
Nimechukizwa
sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka,
Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye
nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia
njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao
katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia,
kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
Sitaki
kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya
madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi
huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana
usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa
MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na
vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.
Serikali
kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni
nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna
mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa
viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa 'agente provocateure' kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
Nimemuomba
Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu
sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika.
Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe
eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. 'An injury to one,
injuries to all'
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.