Trafiki akiwa na wananchi mbele ya mwili wa mtu aliyegongwa na gari na kufa (aliyefunikwa khanga).
Majira ya saa moja kamili asubuhi ya leo mitaa ya Bamaga jirani na
ofisi za gazeti hili mtu mmoja alipoteza maisha papo hapo baada ya
kugongwa na gari wakati akiwa anavuka barabara.Mtu huyo ambaye hakufahamika jina mara moja aligongwa na gari aina ya Toyota Coaster lifanyalo safari zake Mwenge –Posta, kwa mujibu wa shahidi mmoja ambaye hata hivyo alisema hakumbuki namba.
(PICHA HABARI NA HARUNI SANCHAWA/GPL)