Friday, May 18, 2012

MSAFARA WA MAFISANGO AKIPELEKWA DAR AIPORT


Askari akiwapangua waombolezaji kupisha njia kwa ajili ya magari kupita.

Magari yaliyoongoza msafara huo kuelekea uwanja wa ndege.

Gari lililobeba mwili wa marehemu Mafisango, likiwa limezingirwa na mashabiki.

Mashabiki wakikimbiza magari.

Baada ya mashabiki kuuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya soka ya Simba, Patrick Mafisango, katika uwanja wa TCC Chang'ombe uliopo Temeke jijini Dar es Salaam, ulianza msafara kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyereree, ambapo utalala na kesho asubuhi kusafirishwa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya maziko.


Picha/stori na Gladness Mallya / GPL