TAARIFA: Wananchi wa Tanzania, kwa juhudi zao tena, kwa mara nyingine tena, wamegundua utajiri wa madini mara hii ikiwa mkoani Kigoma. Hakuna uvivu, wamelivamia eneo hilo lililotengwa kwa ajili ya shule ya sekondari na hivi sasa uchimbaji wa mali mpya unaendelea. Angalia picha hiyo hapo chini.
Baadhi ya wachimbaji wadogo zaidi ya 1,000 waliovamia kijiji cha Kinyinya wilayani Kibondo mkoani Kigoma wakiendelea na kazi ya uchimbaji na utafutaji madini. Machimbo hayo mapya yaligunduliwa mwezi uliopita katika eneo ambalo lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari na soko kijijini hapo. (Picha na Fadhili Abdallah). SOURCE Habari Leo, Jumatano, April 4, 2012. |