Mama mzazi wa marehemu Steven Charles
Kanumba, Bi. Flora Mtegoa (katikati) akisaidiwa na waombolezaji kuingia
ndani alipowasili nyumbani kwa mwanae Vatican, Sinza jijini Dar
akitokea Bukoba mkoani Kagera.
Mama mzazi wa msanii mahiri wa filamu
nchini, marehemu Steven Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia Jumamosi
nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam, Bi Flora Mtegoa,
jana mchana aliwasili jijini Dar akitokea Bukoba alipokwenda kumjulia
hali mama yake mzazi anayeishi Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera.
PICHA NA SHAKOOR JONGO/GPL
Kwa Hisani ya GPL.