Tuesday, April 10, 2012

KANUMBA ALIVYOAGWA VIWANJA VYA LEADERS DAR

Matayarisho ya kuuombea mwili wa Kanumba yakifanyika.
Jeneza la mwili wa Kanumba likiwasili  Viwanja vya Leaders.
Sehemu ya umati uliofika hapo.
Baadhi tu ya watu waliodondoka na kupoteza fahamu.
Mmoja wa wanakamati ya mazishi, Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (kulia) akimsaidia mama mzazi wa Kanumba (katikati) kwenda kwenye kiti chake.
Mama Salma Kikwete akiwa na waombolezaji.
Makamu wa Rais, Gharib Bilal (kushoto) na Waziri wa Habari na Utamaduni Emmanuel Nchimbi wakiwa msibani.
Msanii wa maigizo, Steven Nyerere anayecheka (kulia) akiwa na Wence Mtuhi (mwenye miwani) ambaye alitoa magari yake kuchukua mwili wa Kanumba.
Baadhi ya wasanii waliofika hapo.
Waombolezaji wakisubiri msafara wa Bilal upite.
Msanii wa filamu Mahsen ‘Dk. Cheni’ akiteta jambo na Wence Mtuhi.
UMATI mkubwa ulijitokeza leo asubuhi katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini hayati Steven Kanumba.

Watu wengi, hususan kina mama waliangua vilio mwili huo ulipopita mbele yao na wengine kudondoka na kupoteza fahamu, hali iliyosababisha watu wa huduma ya kwanza kuwa katika kazi kubwa.

(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)/GPL