Tuesday, March 20, 2012

MMOJA AFARIKI, 14 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI LA PRINCE MURO HUKO SENJELE-TUNDUMA

Basi la Prince Muro baada ya kupata ajali.
Sehemu ya ndani ya basi hilo baada ya ajali.
Hali ilikuwa hivi baada ya ajali.
Mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo aiitwae, Andendekisye akiwa katika Hospitali ya Ifisi jijini Mbeya.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ifisi, Dkt. Mbilinyi akiongea na mmoja wa majeruhi leo asubuhi.
Lori ambalo basi la Muro lilijaribu kulipita na kupata ajali.
----
BASI la Prince Muro lenye namba za usajili T485 BQV jana usiku lilipata ajali mbaya wakati lilipotaka kulipita lori lenye namba za usajili T 664 ABB maeneo ya Senjele, likitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma.
Majeruhi ambao wamenusurika katika ajali hiyo mbaya wamesema, dereva huyo alikuwa mwendo kasi tangu wapo maeneo ya Mikumi Morogoro na kuendelea kudai kuwa walimpa onyo mara kadhaa lakini hakuweza kuwasikiliza na akaongeza mwendo zaidi mpaka walipopata ajali hiyo maeneo ya Senjele, Tunduma.
Chanzo: MBEYA YETU BLOG