Tuesday, January 24, 2012

Rais Jakaya Kikwete,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika Wa Bunge Anne Makinda Na Viongozi Mbalimbali Washiriki Mazishi Ya Aliyekua Mbunge Wa Arumeru(CCM)Jeremia Sumari

Wananchi wa Arumeru kwa kushirikiana na vijana wa UVCCM taifa wakiufukia mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru mashariki Mhe. Jeremia Sumari wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha. Nyuma ni Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Spika mtaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha
 Spika  wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimfariji mke wa Marehemu Mweshimiwa Jeremia Sumari, Bi. Miriam Sumari kabla ya mazishi ya marehumu sumari kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha Leo.Picha Zote na Owen Daudi.


chanzo na http://www.hakingowi.com/