Tuesday, January 17, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU REGIA MTEMA KARIMJEE DAR LEO

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.


Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakiagana na wanafamilia ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Regia  leo januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.

Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Andrew Chenge pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia,  wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Tundu Lissu, Vita Kawawa, pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo.

Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR