Wednesday, April 13, 2011

Mwanamke Achapwa Hadharani kwa Kuzini


Mwanamke Achapwa Hadharani kwa Kuzini

http://api.ning.com:80/files/20YfWB7mnE8V8goRXg5K7H6d7gwmPPZeaAENuRDOUlb0yApzIxFPVlLW5-USpvIQccSmatqzQ4elm*iK1k66KxuWfuoK9FkS/CANINGIIII.jpg
Gazeti la Jakarta Globe linaripoti kwamba mwanamke mmoja raia wa Indonesia amechapwa bakora mbele ya msikiti baada ya kukutwa na hatia ya kufanya tendo la ndoa katika kipindi ambacho alikuwa katika harakati za kuhitimisha talaka yake toka kwa mumewe wa awali.
Irdyanti Mukhtar, 34, alitandikwa bakora tisa kwa kosa la uzinzi mbele ya kadamnasi ya watu 200 waliokuwa wakishangilia kwa nguvu nje ya msikiti wa Al Munawwarah, katika mji wa Jantho.
Mukhtar alihukumiwa siku moja kabla na mahakama ya Kiislamu inayoendesha shughuli zake kwa msingi wa Sharia. Mwendesha mashtaka alisema Mukhtar alikutwa akiwa na mahusiano ya karibu na mwanaume mwingine angali bado kukamilisha talaka yake kwa mumewe wa awali.
Gazeti hili linaendelea kuripoti kwamba mama huyu alikuwa ni mmoja kati ya watu wanne, akiwemo mwanaume anayesemekana kuzini nae, kutumikia adhabu hiyo ya viboko.
Polisi ambao pia wanafanya kazi chini ya mfumo wa Sharia wanafanya uchunguzi juu ya tuhuma za mama huyu kwamba alidhalilishwa na kadamnasi kabla ya kufikishwa mahakamani.
Mara baada ya kumaliza kupokea adhabu hii ya viboko mama huyu alipoteza fahamu na alikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Unaweza kutazama picha za adhabu hii hapa chini:
http://i.huffpost.com/gen/265665/CANING-III.jpg?width=500
http://i.huffpost.com/gen/265661/CANING-I.jpg?width=500