Tuesday, March 22, 2011

Ajali haina kinga

Ndugu Mkuu wetu,

Tunaomba uangalie maisha ya Watanzania maana hizi ajali za Barabarani zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku.

Mwito kwa madereva wote, unapoendesha chombo cha moto tafakari athari zake na pia jua hauko pekee yako.

Kuna watembea kwa miguu, kuna abiria, kuna wanyama pia kuna madereva wenzako. Chukua tahadhali kila wakati na chunga maisha ya wenzako.


Hiyo ni ajali mbaya ambayo imeghalimu maisha ya Watanzania wenzetu.

Japo tunajua kifo ni njia ya kila mmoja lakini tunapaswa kuchukua tahadhali wakati mwafaka.

Globu hii ya Hapa na Pale katika maisha inawapa pole wafiwa wote na Watanzania kwa ujumla.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.