Niliwahi kufanya mahojianao na baadhi ya waajiri ambao wanatoka nchi mbalimbali tena nyanja mbalimbali,wengi wao walisema ni nadra sana kwake kuangalia kurasa zaidi ya pili ya CV,waajiri hupendela na kutamani CV fupi,najua kuna baadhi yetu wanaweza kuwa na mtazamo tofauti juu ya hili,hivyo leo nitatoa muono wangu halafu mlango umefunguliwa kwa wenye maoni wachangie.
Je unaijua CV?:
Kiufupi ni kuwa CV haitakiwi iwe na kurasa nyingi,hii ni kwa sababu hii ni CV na sio utambulisho binafsi (autobiography).Wengi wamesahau kuwa hautapata kazi kupitia CV yako bali utapata nasafi ya kufanyiwa usaili(interview) kutegemeana na CV yako, matokeo yake ni kupata ajira kulingana na nini ulichokifafanua kwenye usaili.Kumbuka kwenye usaili ndio uwanja wako wa kujidai ambapo utwaweza kufafanua kwa mapana na marefu huku ukijidai kwenye fani yako.
Uzoefu wa kazi:
Kuna wengi wanaamini kuwa jinsi anavyoorodhesha uzoefu wake ndivyo anavyowavutia waajiri,hili halina ukweli isipokuwa kama huo uzoefu wako una uhusiano na kazi iliyopo mkononi.Ndio maana watu husema andika CV inayoendana na kazi husika.Maharage yanaweza kuwa ni mboga kwa mtanzania ila sio kwa mchina.Hapa nina maana uzoefu wako kama daktari hauna msaada kwenye kazi ya kunyanyua mizigo bandarini.Wengi wetu tumekuwa tukichanganya juu ya nini ni muhimu kwako na nini ni muhimu kwa waajiri na ni jinsi gani utaunganisha mawazo uako na ya muajiri.
Majukumu:
Cha msingi kukumbuka pindi uandikapo CV yako ni kuweka bayana nini umefanya(accomplishments) na sio kazi zako(duties).Vilevile weka akilini kuwa lazima uhakikishe unazifikisha kwa undani wake.Kwani waajiri hupenda sana kuuliza nini utafanya na sio nini umesoma au unacho kwenye cv.Kwa mfano labda wewe ni mtoa msaada(tech supporter) wa kampuni A,unatakiwa kufafanua pindi ulipokuwa kampuni A uliweza vipi kupunguza mlundikano wa matatizo,uliweza vipi kuongeza ubora wa huduma kwa wateja,je wateja walinufaika vipi na nini maoni yao siku ya mwisho? Mambo kama haya na mengine mengi yanaweza kuwa na msaada mkubwa kwako pindi uandikapo CV yako.
Labda nikupe ujanja ambao unaweza kuwa na msaada kwako,baada ya kumaliza kuandika CV yako na kuelezea nini ulifanya kwemnye kampouni fulani,jiulize mwenyewe,”SASA”??? Hii itakusaidia kujiweka kwenye nafasi ya muajiri na kufikiria kama muajiri? Ingawa ni ngumu kupata mchanganuo wote ila utaweza kupata picha ya mchezo kamili.
Suluhisho:
Kitu cha msingi ambacho leo nimegawana nanyi wana AfroIT ni kuwa,jaribu kufupisha CV yako,andika CV inayojiuza na kujiongoza,usiwachoshe waajiri na kufanya waanze kukuchukia au kukushusha kiwango.Baada ya kuandika CV yako,jaribu kuomba ushauri toka kwa watu mbalimbali walio kwenye hiyo idara.