Wednesday, October 20, 2010

Nafasi za kazi UtumishiTanzania za Kumwaga

NAFASI ZA KAZI UTUMISHI TANZANIA

MWANANCHI JUMATATU OKTOBA 18,2010

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
KUMB. NA AC.13/231/01
NAFASI ZA KAZI

Sekretariati ya ajira katika utumishi wa umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika utumishi wa umma kwa niaba ya waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma anakaribisha maombi ya watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kwa waajiri mbalimbali katika utumishi wa umma.

1. AFISA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – (NAFASI 1)
2. MCHAPA HATI DARAJA LA II – ( NAFASI 5)
3. MTAKWIMU DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II)- (NAFASI 10)
4. AFISA MICHEZO DARAJA LA II ( GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II) – (NAFASI 15)
5. AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI – (NAFASI 100)
6. MHADROLOJIA DARAJA LA II ( GYDROLOGIST GRADE II) – (NAFASI 35)
7. AFISA KAZI II (LABOUR OFFICER II) – ( NAFASI 30)
8. MHAIDROJIOLOJIA DARAJA II (HYDROGEOLOGISTS GRADE II) – ( NAFASI 5)
9. FUNDI SANIFU DARAJA LA II ( TECHNICIAN GRADE II) – HAIDROLOJIA – (NAFASI 88)
10. FUNDI SANIFU DARAJA LA II ( TECHNICIAN GRADE II) – HAIDROJIOLOJIA – (NAFASI 90)
11. MJIOLOJIA DARAJA LA II (NAFASI 4)
12. MHANDISI DARAJA LA II (NISHATI) – (NAFASI 4)
13. MHANDISI DARAJA LA II(MITAMBO) – (NAFASI 2)
14. MHANDISI DARAJA LA II – BAHARINI (MARINE ENGINEER) – (NAFASI 2)
15. MHANDISI DARAJA LA II ( UJENZI) – (NAFASI 10)
16. FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UJENZI) – (NAFASI 32)
17. FUNDI SANIFU II(UFUNDI UMEME) – (NAFASI 30)
18. FUNDI SANIFU II – MITAMBO YA BARAFU (REFRIDGERATION TECHNICIAN) 0 (NAFASI 7)
19. FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UFUNDI NA UMEME) NAFASI 2
20. AFISA MAENDELEO YA JAMII DARAJA II – (NAFASI 20)
21. AFISA UGAVI MSAIDIZI – (NAFASI 146)
22. AFISA ARDHI DARAJA LA II – (NAFASI 10)
23. MPIMA ARDHI DARAJA LA II – (NAFASI 32)
24. AFISA MIPANGO MIJI DARAJA LA II - ( NAFASI 15)
25. MTHAMINI DARAJA LA II – (NAFASI 1)
26. MKADIRIAJI UJENZI DARAJA LA II (QUANTITY SURVEYOR GRADE) – (NAFASI 10)
27. MSANIFU MAJENGO (ARCHTECT ) DARAJA LA II – (NAFASI I)
28. AFISA ARDHI MSAIDIZI – (NAFASI 5)
29. FUNDI SANIFU DARAJA LA II – (NAFASI 35)
30. FUNDI SANIFU II (TUTOR) – (NAFASI 4)
31. AFISA MISITU DARAJA II – (NAFASI 15)
32. AFISA USAFIRI DARAJA LA II – ( NAFASI 5)
33. AFISA UVUVI DARAJA LA II – (NAFASI 5)
34. MVUVI MSAIDIZI DARAJA LA II – (NAFASI 37)
35. MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II (NAFASI 27)
36. AFISA UFUGAJI NYUKI II – (NAFASI 6)
37. MSAIDIZI UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II – (NAFASI 12)
38. KATIBU WA KAMATI DARAJA LA II – (NAFASI 8)
39. MKAGUZI WA MJI – (NAFASI 11)
40. MPISHI DARAJA LA II – (NAFASI 7)
41. DOBI DARAJA LA II – NAFASI 5
42. MHUDUMU WA JIKONI/MESS DARAJA LA II – (NAFASI 30)
43. AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – (NAFASI 135)
44. AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III – (NAFASI 34)
45. AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II – (NAFASI 5)
46. AFISA TARAFA – (NAFASI 12)
47. AFISA MTENDAJI MTAA II (NAFASI 10)
48. MKUTUBI DARAJA LA II (NAFASI 5)
49. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NYARAKA) – NAFASI 30
50. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III – NAFASI 182
51. MPOKEZI – (NAFASI 6)
52. MSAIDIZI WA MAKTABA DARAJA LA II ( NAFASI 10)
53. MSAIDIZI WA OFISI – NAFASI 44
54. MLINZI - NAFASI 204
55. DEREVA MITAMBO DARAJA LA II – NAFASI 1
56. DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II – NAFASI 9
57. DEREVA DARAJA LA II – (NAFASI 276)
58. MHADHIRI MSAIDIZI (ASSISTANT LECTURER) – NAFASI 1
59. MHADHIRI MSAIDIZI (ASSISTANT LECTURER) – NAFASI 2
60. AFISA UTUMISHI MWANDAMIZI (NAFASI MOJA)
61. MKAGUZI WA HESABU WA NDANI DARAJA LA III (INTERNAL AUDITOR GRADE III – NAFASI 1)
62. AFISA MITIHANI MWANDAMIZI II (NAFASI 1)
63. MTAALAMU WA MIFUMO YA TAARIFA II – DATA BASE ADMINISTRATOR (NAFASI 1)
64. MCHAMBUZI WA MIFUMO (SYSTEM ANALYST) – NAFSI 1
65. MPIGA CHAPA MSIMAMIZI II (PRINTING SUPERVISOR ) NAFASI MOJA
66. MPIGA CHAPA MWANDAMIZI II (SENIOR PRINTER) NAFASI MBILI
67. MPIGA CHAPA MWANDAMIZI II (SENIOR BINDER) NAFASI MBILI
68. MPIGA CHAPA MSIMAMIZI II (BINDING SUPERVISOR ) NAFASI MOJA
69. KATIBU MAHUSUSI DARAJA LA I NAFASI 3
70. KATIBU MAHUSUSI DARALA LA II NAFASI 1
71. MLINZI MWANDAMIZI NAFASI 3
72. FUNDI SANIFU MKUU NAFASI 1
73. FUNDI SANIFU MWANDAMIZI
74. AFISA MILIKI II (ESTATE OFFICER) NAFASI 1
75. MHASIBU II NAFASI 2
76. MPIMAJI HALI YA HEWA MSAIDIZI (METEOROLOGICAL ASSISTANTS II) – NAFASI 45
77. MCHAMBUZI WA MIFUMO YA KOMPYUTA (SYSTEM ANALYST II ) – NAFASI 1
78. MUUNDAJI WA PROGRAM ZA KOMPYUTA (COMPUTER PROGRAMMER) – NAFASI 1
79. MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT II) – NAFASI 1
80. AFISA UHUSIANO ( PUBLIC RELATIONS OFFICER II) - NAFASI 1
81. MKAGUZI WA HESABU ZA NDANI II (INTERNAL AUDITOR II) NAFASI 2
82. AFISA UHUSIANO NA MASOKO MWANDAMIZI (NAFASI 1 ) SENIOR PUBLICITY AND MARKETING OFFICER
83. MENEJA MIPANGO (NAFASI 1) PLANNING MANAGER
84. MRATIBU WA MITAALA – SOMO LA HISTORIA (NAFASI 1) CURRICULUM COORDINATOR
85. MHASIBU MKUU DARAJA LA II (NAFASI 1) – PRINCIPAL ACCOUNTANT
86. MHASIBU MSAIDIZI (NAFASI 1) ASSISTANT ACCOUNTANT
87. DEREVA MWANDAMIZI (NAFASI 1)


MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE
1. Waombaji wawe raia wa Tanzania
2. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa
3. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa umma, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
4. Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) pamoja na klpicha moja ya passport size ya hivi karibuni iandikwe jina.
5. Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji waonyeshe anwani na namba za simu za kuaminika.
6. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.viambatansisho hivyo vibanwe sawasawa kukondoa uwezekano wa kudondoka na kupotea. “Testmonials”, “Provisional Results.” “Statement of Results” HAVITAKUBALIWA.
7. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45
8. Waombaji waliostaafishwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha katibu mkuu kiongozi
9. Aidha matangazo haya yanapatikana kwenye tovuti zifuatazo:- www.utumishi.go.tz na pmoralg.go.tz.
10. Waajiri wote waliopo nje ya Dar es salaam wanaombwa kusambaza matangazo haya kwenye mbao za matangazo na maeneo mengine.
11. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tareh 5 Novemba, 2010, baada ya Tangazo hili kutoka gazetini kwa mara ya kwanza.
12. Maombi yanaweza kuandikwa kawa lugha ya Kiswahili au kiingereza na yatumwe kupitia anuani ifuatayo:-

Katibu,
Sekretariati ya ajira katika utumishi wa umma,
SLP 63100,
Dar es salaam.

AU

Secretary,
Public Services Recruitment Secretariat,
P.O.BOX 63100
Dar es salaam.