Saturday, October 16, 2010

Mgombea Chadema afanyiwa Fujo Masama

 Jamani Watanzania amani lazima izingatiwe na watu wote. Hatutaki fujo sasa hawa walioko madarakani wanaweza kweli kukubali matokeo kwa style hii? Tunaomba Amani ndugu zangu Watanzania, soma hapo chini uone jinsi wafuasi wa vyama vyetu wanavyofanya mambo yasiotakanika.


Ilikuwa kama sinema za akina Rambo ama matukio ya Rwanda Genocide.
Mgombe wa ubunge jimbo la Hai kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe
akiwa katika mkutano wa hadhara huko Masama Kati ghafla kijana mmoja
wa Green Guard alivamia mkutano kwa lengo la kuanzisha fujo. Kikosi
cha ulinzi cha CHADEMA kilimdhibiti kijana huyo na kumhifadhi katika
gari moja kwa lengo la kupisha mkutano uendelee.

Kumbe kijana huyo alikuwa ametangulizwa tu na kwamba pamoja naye
walikuwepo vijana wa Green Guards wasiopungua 100. Vijana hawa
wakiongozwa na Mgombea udiwani wa CCM katika kata hiyo walikwenda
kufunga barabara ili msafara wa Freeman usipite eneo hilo. Kwa kawaida
msafara wa Mbowe hutanguliwa na pick-up ambayo hubeba jukwaa na viti.
Vijana hawa wa CCM waliliteka gari hilo lililokuwa linaendesha na Ndg.
Lootore Lema na kumchukua kumpeleka katika nyumba ya mwanaCCM mmoja
katika eneo hilo la Masama Mbweera.

Mbowe kusikia kuwa kamanda wake ametekwa alivunja mkutano na kuondoka
kwenda kumwokoa. Walipofika kama 200m toka eneo la mkutano walikuta
jeshi kubwa la vijana wa CCM wakiwa wameshikilia mapanga, mawe,
majembe na vyuma. Hapo vita kamili ikaanza.

Katika vita hiyo magari ya msafara wa Mbowe yapatayo 6 yamevunjwa
vunjwa vioo. Wanachama wa CHADEMA wameumizwa. Hata hivyo vijana wa
CHADEMA walijitahidi kumlinda mwenyekiti wao wa taifa kwa kuongoza
mapigano kama vita vya kawaida kabisa vya msituni. Ilimlazimu
Mheshimiwa Mbowe kutoa bastola yake na kufyatua risasi kadhaa hewani
ndipo Green Guards waliporudi nyuma na hivyo kuwezesha kupunguza kwa
kiasi kikubwa madhara ambayo yangetokea kwa vita hiyo kuendelea uso
kwa uso.

Ilikuwa patashika. Walinzi wa Mbowe walikuwa wakiwafuata Green Guards
na kuwanyang'anya silaha zao na kuzitumia kuwapiga nazo. Kwa nasibu
vijana kadhaa wa CCM wamekamatwa na kwa sasa wako katika kituo cha
polisi cha wilaya ya Hai kwa ajili ya kuandika maelezo.

Taarifa zilizonifikia punde zinasema kuwa kijana mmoja ambaye amepigwa
vizuri na CHADEMA ameomba asidhuriwe zaidi kwani atasema yote; namna
walivyotumwa kuvamia na kuharibu mikutano ya Mbowe.

Waheshimiwa haya ni matunda ya mafunzo ya kijeshi ambayo CCM
waliyafanya kwa vijana wao wapatao 5000 huko Iringa mwezi March mwaka
huu na baadaye kule Moshi Vijijini ambako walitoa mafunzo ya kijeshi
kwa vijana 350.

Chonde Chonde CCM!!
Madaraka mnayataka, Sawa; Lakini Damu yetu mnaitakia nini?
TUACHIENI AMANI YETU!!!!!!!!!

--
Wanabidii wanakutana Tarehe 20/10/2010 Peacock kwa habari zaidi piga 0787984842

Kama una malalamiko tuma wanabidii@gmail.com