Huenda Jambo Kubwa sana ulilojua kuhusu uchaguzi wa Gambia ni Kuondolewa kwa Kiongozi Nguli wa Nchi Hiyo Yahya Jameh na sana kama unafuatlia medani za siasa katika duru la Kimataifa utagundua pia kwamba Gambia ilikataa katu kuruhusu waangalizi wa umoja wa Ulaya bila kutoa sababu zozote....hata hivyo Waangalizi kutoka Muungano wa Afrika (AU), Jumuiya ya Madola na Jumuiya ya mataifa ya kiislamu OIC waliruhusiwa.
UCHAGUZI wa Taifa dogo la Afrika Magharibi la Gambia lililopo kilometa chache ukingoni mwa Jangwa la Sahara, uligubikwa na mvuto wa kipekee kutokana na wasifu wa wagombea wawili waliochuana vikali. Rais aliyebwagwa katika uchaguzi huo, Yahya Jammeh, aliyetawala kwa miongo miwili na ushei aliyeingia madarakani kwa Mapinduzi ya kijeshi amekubali kushindwa na kuahidi kukabidhi madaraka kwa amani kwa mpinzani wake aliyeshinda, Adama Barrow, ambaye hajawahi kuongoza katika ngazi yoyote ya kisiasa.
Wagombea wote wawili wanawiana kwa umri (miaka 51) ambapo Jammeh aliyeingia madarakani kwa Mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu mwaka 1994 alijipatia asilimia 36 ya kura zote zilizopigwa, Barrow alijipatia asilimia 45 na mgombea wa tatu Kandeh alijipatia asilimia 17.8.
Pengine matokeo hayo yaliyopokewa kwa nderemo na vifijo si kivutio kikubwa zaidi cha uchaguzi, lakini ni mfumo mbadala wa Taifa hilo katika kupiga kura unaotofautiana na mataifa mengine kwa kutotumia kadi za kupiga kura bali kinachotumika ni gololi zisizokuwa na rangi wanazotumbukiza wapiga kura katika pipa lenye rangi inayomwakilisha mgombea wanayetaka kumchagua.
Kuanguka kwa gololi hiyo ndani ya kitako cha pipa na kutoa sauti ya kugonga humwezesha msimamizi wa uchaguzi kutambua endapo mpiga kura yeyote atajaribu kupiga kura zaidi ya moja anayopaswa kutumbukiza.
Ni mfumo ulioanza kutumika mwaka ambao wagombea Jammeh na Barrow walizaliwa (1965), kutokana na kiwango duni cha elimu miongoni mwa Wagambia wengi ambao wasingeweza kutumia mfumo uliozoeleka unaohusisha kuandika.
(Asilimia 49 ya Wagambia hawajui KUSOMA WALA KUANDIKA PIA)
Kutokana na upande wa chini kwa ndani ya pipa kutoa sauti inayorandana na kengele ya baiskeli siku ya kupiga kura hairuhusiwi kuja na baiskeli katika kituo cha kupiga kura ili kutosababisha mkanganyiko. Mapipa hayo huwekwa sanjari ili isiwezekane kuinua mojawapo na kubaini matokeo kabla ya kuhesabiwa kutokana na uzito kwa wingi wa gololi, kila pipa hupakwa rangi ya chama cha mgombea na kuwekwa jina la chama anachowakilisha na picha ya mgombea.
Baada ya kupiga kura mpiga kura huchovya kidole katika wino kuthibitisha kuwa ameshiriki katika kupiga kura. Katika kuhesabu kura gololi hizo huwekwa kwenye ubao wenye vishimo kati ya 200 hadi 500 ili kurahisisha kazi ya kuhesabu.
......Yaani hakuna kubishana AMA UTATA kuhusu peni sijui imefanyaje ..
Ama badu, uchaguzi wa Gambia ambao umeshtua wengi umegubikwa na hisia nyingine ikiwemo ya watu kutoamini kwamba Jammeh angekubali kuachia madaraka kirahisi (ALIWAHI KUSEMA watu wakimchagua hata miaka bilioni ataongoza tu ma akishindwa atarudi shambani) dhidi ya mpinzani wake ambaye licha ya kutojulikana kwenye duru za siasa pia alikua MLINZI NA DALALI tu na sasa ni RAIS WA NCHI
Jammeh ameiongoza Gambia kwa takribani miongo miwili (miaka 22).
Rais Yahya Jameh anastahili pongezi kubwa kwa kukubali matokea na kumpongeza mpinzani wake - hili na jambo nadra sana hapa Afrika. Watu wengi walitegemea atatumia mbinu abakie madarakani na vyombo vya habari vya magharibi vilikua mbele kumpa kila sifa mbaya.
Na Geofrey Chambua
Kutoka Vyanzo Mbalimbali