Tuesday, October 04, 2016

RC Makonda azitaka taasisi na mashirika ya umma kutumia TTCL


RC Makonda azitaka taasisi na mashirika ya umma kutumia TTCL
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka taasisi na mashirika ya umma yaliopo chini ya mkoa wake kuiunga mkono Kampuni ya Simu ya kizalendo Tanzania (TTCL) kwa kuanza kuzitumia bidhaa za kampuni hiyo hasa kwenye shughuli za mawasiliano ili kuonesha uzalendo kwa vitendo. 

Makonda ametoa kauli hiyo leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa kampuni ya TTCL, huku akiahidi kuzishawishi taasisi na mashirika ya umma yanayofanya kazi chini ya utawala wake kuhakikisha wanatumia huduma za TTCL ili kuiunga mkono kampuni hiyo ya kizalendo ya mawasiliano. 

Alisema Serikali imeonesha nia njema ya kuirejesha TTCL katika hali nzuri baada ya kuirejesha kwa asilimia 100 chini ya umiliki wake, hivyo kuyataka mashirika na taasisi za umma kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kuirejesha kampuni hiyo chini ya umiliki wa serikali kwa asilimia 100. 

Alisema yete kama kiongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam atahakikisha ofisi zote za umma zilizopo chini ya mkoa wake zitatumia huduma za TTCL na endapo watendaji wa TTCL sinazosita kutumia watoe taarifa ili yeye ahoji ni kwanini wanapinga agizo hilo. 
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) wakigonganisha glasi za mvinyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na mwenyeji wake huku akionesha alama ya mabadiliko inayotumiwa na TTCL.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI