Thursday, August 11, 2016

TANZANIA YATAJWA MIONGONI MWA NCHI ZINAZOFANYA VIZURI KATIKA UWEZESHAJI WA WANAWAKE



TANZANIA YATAJWA MIONGONI MWA NCHI ZINAZOFANYA VIZURI KATIKA UWEZESHAJI WA WANAWAKE
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kwa mujibu wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake.
Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika kushughulikia masuala ya wanawake kupitia Sera zilizopo nchini humo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (kushoto) ambaye ni miongoni mwa wanawake viongozi wa Tanzania walionufaika na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation akizungumza jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa hafla fupi ya Tathmini ya Mafanikio ya Mfuko wa Hanns Seidel Foundation nchini Tanzania, jana usiku jijini Dar es salaam.
Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko huo jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake.
Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller (kulia) akifurahia picha ya kuchorwa aliyokabidhiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) jana jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kushoto ni Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani, jana jijini Dar es salaam.

Na.Aron Msigwa – Dar es salaam.

Mfuko wa Hanns Seidel Foundation (HSF) unaojihusisha na uwezeshaji wa wanawake katika nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali umeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake duniani.

Mwenyekiti wa Mfuko huo ambao makao yake yako nchini Ujerumani Prof. Prof.Ursula Mannle ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati hafla fupi iliyoandaliwa na mfuko huo kwa lengo la kufanya tathmini ya mchango wa HSF nchini Tanzania katika kuwajengea uwezo wanawake vijana katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa.

Prof. Ursula amesema kuwa HSF imekuwa ikitekeleza program mbalimbali za uwezeshaji kwa wanawake kisiasa, kuwaandaa na kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi mahiri katika nchi wanazotoka.

Amesema HCF imeamua kuanzisha programu maalumu nchini Tanzania kwa ajili ya kuwaangalia wanawake wanaojitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi ili kuwawezesha kuwa viongozi katika nafasi mbalimbali serikalini pia kuziba pengo lililopo la uwakilishi katika nafasi za kisiasa.

Ameeleza kuwa Hanns Seidel Foundation itaendelea kuwaunga mkono wanawake wa Tanzania wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania kupitia program mbalimbali za ufadhili ili kuwawezesha kumudu gharama na kuwajengea uwezo wa kushindana katika majukwaa ya Siasa.

Waziri Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla hiyo amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa kipaumbele katika nafasi za uongozi kwa wanawake.

Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake vijana wa Kitanzania zikiwemo za kijamii na kimila pia ndoa na mimba za utotoni zinazochangia vijana wanafunzi wa kike kuacha masomo yao, Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuja na Sera ya Elimu bure kuwawezesha vijana wa kike wa kitanzania kupata elimu.

Amesema Tanzania imeendelea kuwathamini wanawake katika uteuzi wa ngazi mbalimbali za uongozi Serikalini kuanzia wakuu wa Wilaya, Mikoa, Wakurugenzi, Mawaziri na Naibu Mawaziri pia uwepo wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni alama ya hamasa na ushindi katika uongozi kwa wanawake wengine Tanzania.

Mhe. Mwalimu ameushukuru Mfuko huo kwa mchango wake katika kuwainua wanawake wa Tanzania pia program mbalimbali zilizoanzishwa na mfuko huo kwa lengo la kuwawezesha wanawake nchini.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika kushughulikia masuala ya wanawake amesema kuwa kupitia Sera zinazosimamia masuala ya wanawake mambo mengi yameweza kufanyika. 

Ametoa wito kwa Tanzania kuendelea kuzishughulikia changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo kwa wanawake wa Tanzania kufika mbali na kuwazuia wasiweze kusimama wenyewe katika masuala ya Siasa.

Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula ambaye ni miongoni mwa wanawake wa Tanzania walionufaika kutokana na HSF amesema kuwa alianza harakati za siasa mwaka 2004 licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.

Amesema kuwa ipo haja ya wagombea wanawake vijana wanaoingia katika ulingo wa siasa kusaidiwa kifedha na mfuko huo pamoja na vyama vyao vya siasa wanavyoviwakilisha pindi wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuongeza kuwa wakati umefika kwa wanawake wanaoingia katika siasa kusimama wenyewe kwenye majimbo ya uchaguzi.

Ametoa wito kwa HSF kuendelea kuwasaidia wanawake vijana wanaoingia kwa mara ya kwanza katika masuala ya siasa kwenye chaguzi zinazokuja ili kuwawekea mazingira mazuri ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.