Tuesday, July 05, 2016

VIFUNGO GEREZANI BILA FAINI, NA SI VITOCHI VYA TRAFIKI, NDIO DAWA YA KUPUNGUZA AJALI BARABARANI



VIFUNGO GEREZANI BILA FAINI, NA SI VITOCHI VYA TRAFIKI, NDIO DAWA YA KUPUNGUZA AJALI BARABARANI
 Mabasi yakifukuzana mlima wa Kitonga kuelekea Iringa. Wananchi wengi waliohojiwa na Globu ya Jamii wamependekeza kuwepo na adhabu ya kifungo gerezani moja kwa moja bila kuwepo na faini ya aina yoyote kwa dereva wa mabasi ya abiria na magari mengine kwa kosa lolote lenye kuhatarisha maisha ya watu. Wananchi hao wametolea mfano njia za mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es salaam ambapo wananchi hivi sasa wanaziheshimu njia za mabasi hayo baada ya watu kadhaa kupewa adhabu ya vifungo gerezani bila faini.
Alama barabarani hapo zinamaanisha HAKUNA KUPITA KABISA lakini dereva wa basi anapuyanga tu, tena kwenye kona kona za mlima Kitonga.