Sunday, April 03, 2016

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO,PROFESA MAKAME MBARAWA AONGEA NA WAFANYAKAZI WA TAASISI ZA WIZARA HIYO WA MKOA WA KIGOMA NA KATAVI



WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO,PROFESA MAKAME MBARAWA AONGEA NA WAFANYAKAZI WA TAASISI ZA WIZARA HIYO WA MKOA WA KIGOMA NA KATAVI

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akiangalia namna mkongo wa Taifa ulivyopitishwa katika moja ya madaraja ya Mto Malagarasi. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Kamugisha Kazaura akiangalia kwa makini.
 Wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakimsikiliza Waziri wa Wizara Prof. Makame Mbarawa, (hayupo pichani), wakati alipoongea nao mkoani Katavi.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiongea na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo wakati akifanya majumuisho ya ziara yake, mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tano kutoka kulia mstari wa kwanza), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoani Kigoma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.