Fundi wa ujenzi akimwaga kifusi katika kipande cha barabara hiyo ili kusaidia iweze kupitika kwa urahisi kutokanana kuharibiwa vibaya na mvua. |
Mansipaa ya Temeke imetenga kiasi cha sh bilioni 1.5 kwa mwaka huu wa fedha wa 2016/2017 kwa ajili ya ujenzi, kiwango cha lami kipande cha barabara ya Mbosi chenye urefu wa kilometa 1.3 kinachopiota nje ya Kiwanda cha Mabati cha Alluminium Africa (ALAF).
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo (jumapili), mkurugenzi wa manispaa ya Temeke, Photidas Kagimbo alisema manispaa yake imetenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kipande hicho cha barabara chenye urefu wa kilometa 1.3.
Alisema ujenzi huo utafanyika baada ya malalamiko ya muda mrefu ya wafanyabiashara wa eneo hilo wakiwemo wamiliki wa viwanda ambako barabara hiyo inapita ikiunganisha ile ya Mbozi hadi barabara ya Nyerere, jirani na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).
Alisema awali walifanya mazungumzo na kiwanda cha ALAF na Steel Masters ili kuangalia jinsi ya kutatua changamoto hiyo na baada ya ufuatiliaji wa muda mrefu hatimaye hivi sasa itajengwa ifikapo mwaka mpya wa fedha 2016/2017.
"Ni changamoto ya muda mrefu lakini sasa imepata ufumbuzi" alisema na kuongeza kuwa awali ilikuwa inajengwa ili iweze kupitika lakini kutokana na shehena za mizigo mizito zinazopitishwa katika barabara hiyo uhai wake unakuwa wakati wa kiangazi na mvua zikinyesha kunakuwa na mashimo makubwa.
Alisema magari yenye mizigo mizito ambayo mengine ni hadi tano 40 ni changamoto kwa barabara hiyo lakini hata hivyo sasa inajengwa kiwango cha lami hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia adha wenye viwanda na pia wafanyabiashara wa soko la Mapambano.
Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti na mandishi wa habari hizi, wafanyabiashara katika soko hilo la Mapambano walidai kuwa wanapata shida hususan siku za mvua kwani magari yamekuwa hayapiti barabara hiyo zaidi ya yale ya mizigo mikubwa.
Magari yakipita kwa shida mbele ya kiwanda cha Mabati cha Alluminium Africa (ALAF), barabara ya Mbosi jijini Dar es Salaam. Barabara hiyo imeharibika vibaya kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa.