Wakazi wa Kata ya Kibamba wamepiga kura ya siri kuwabaini wahalifu wanaoishi katika maeneo yao kufuatia tukio la karibuni la uvamizi katika nyumba nne zilizopo Mtaa wa Muhongoni ambalo limesababisha kifo cha mkazi mmoja wa eneo hilo, aliyejulikana kwa jina la Julius Msalangi.
Upigaji kura huo ulifanyika katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ambao ulifanyika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata na kuhudhuriwa na Kamanda wa Polisi wa Kata ya Kibamba, Pius Lutumo.
Uamuzi wa kupiga kura hiyo umetokana na kuanza kuibuka kwa vitendo vya ujambazi unaofanywa majumbani na makundi ya vijana, uporaji wakati wa alfajiri na wizi wa mifugo hali ambayo imesababisha watu kadhaa kujeruhiwa na wengine kupoteza mali zao.
Katika mkutano huo, wakazi hao walikubaliana na kupiga kura za siri ambazo ziliwataja mara nyingi watuhumiwa wa uhalifu sugu wanne ambao Diwani wa Kata hiyo, alisema hata yeye majina yao ameyakuta ofisini kwake hivi karibuni alipoingia madarakani hivi karibuni.
Diwani wa kata hiyo, Ernest Mgawe aliwataka wakazi wa kata hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na ofisi yake hasa pale yanapotokea matukio ya uhalifu nna kukamatwa kwa watuhumiwa ili lengo la kuifanya Kibamba kuwa sehemu salama ya kuishi liweze kufikiwa.
"Tunaomba ushirikiano wenu kwani kuna wakati watu walivamiwa na kujeruhiwa na mmoja kati ya watuhumiwa sugu ambaye pia leo ametajwa lakini hata hivyo wahanga walipotakiwa kwenda olisi kutoa maelezo ili mlenga afikishwe maakamanbi hawakuonekana" alisema.
Awali Kamanda wa polisi wilaya ya kipolisi ya Kibamba aliwataka wananchi watambue kuwa suala la ulinzi na usalama ipo miononi mwao kutokana na hali halisi ilivyo hvi sasa na kuwataka waachane na nadhjaria kuwa polisi ndi walinzi wao na mali zao.
"Hilo mnapaswa kjulitambua na kulingana na sheria ndogo zilizotungwa katika manuspaa ya ionondoni suala la ulinzi shrikishi sio iyari hasa pa,e wananchi wanapokubaliana upitia mikutano yao halali kma huo" alisema.
Alibainisha kuwa kura za siri zilizopigwa zitafanyiwakazi na kila mkazi ni lazima ashiriki ulinzi huo iwe kwa yeye mwenyewe kutoka na kulinda au kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya uwezeshaji wa mpango huo na wale ambao watakaidi watafikishwa mahakamani kwani sheria ipo wazi.
Pia Diwani Mgawe amewapa siku 30 watu wanaomiliki maeneo katka kata hiyo ambayo hawajayaendeleza hivyo kuwa mapori ambayo sasa yanatumiwa kama maficho ya wahalifu na baada ya muda hup atawasilisha majina kwa mkuu wa mkoa kwa aili ya hatua zaidi.
Alisema kuna maeneo mengi eneo hilo ambayo wamiliki wake hawayaendelezi na yamegeuka mapori na ingawa wengine wana hati za kuyamiliki lakini wataomba msaada ofisi ya mkoa kwa hatua zaidi ili kuwanusuru wananchi na madhila ambayo wanayapata hivi sasa.