Wednesday, March 30, 2016

UBALOZI WA TANZANIA MJINI ROMA KUSAFIRISHA WHEELCHAIRS 100 KWA AJILI YA WATU WENYE ULEMAVU


UBALOZI WA TANZANIA MJINI ROMA KUSAFIRISHA WHEELCHAIRS 100 KWA AJILI YA WATU WENYE ULEMAVU
Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania Roma nchini Italia, Bw. Salvator Marcus Mbilinyi (kushoto) akikabidhiwa baiskeli maalum za watu wenye ulemavu (wheelchairs) 100 (mia moja) kwa ajili ya watu wenye ulemavu nchini kutoka kwa Bw. Ziya Karahan, Konseli wa Heshima wa Tanzania mjini Istanbul, Uturuki. Baiskeli  hizo zimepatikana kufutia mazungumzo kati ya Ubalozi na Konseli wa Heshima kuhusu njia za kuvipata vifaa hivyo ili kuwasaidia watanzania wenye ulemavu na hivyo kufanikiwa kupata 100. Baada ya makabidhiano hayo vifaa hivyo vitasafirishwa mara moja kwenda nchini Tanzania kwa ajili ya matumizi husika.