Mhandisi wa Ndege akitumia mkebe wa vifaa uliokwisha unganishwa kwenye mfumo mpya mbele ya Ndege ya shirika la Etihad aina ya Airbus A330 ambayo ilikuwa inapitia marekebisho ya kawaida.
Wakisimama pembeni ya mikebe ya vifaa iliyounganishwa na mfumo mpya kwenye karakana ni (kutoka kushoto) Isam fares, Meneja GSE, Vifaa na maduka, Michael Adams, Makamu Rais MRO Services, Reinhard Luksch, Mkuu wa Vifaa na Utendaji Kitengo cha uhandisi wa matengenezo ya ndege cha Shirika la Ndege la Etihad.
SHIRIKA la ndege la Etihad kupitia idara yake ya uhandisi limeimarisha uwezo wake wa matengenezo ya ndege na mfumo mpya wa kujiendesha wenyewe moja kwa moja (ATC), mfumo ambao unasaidia wahandisi katika upatikanaji, utunzaji na ufuatiliaji wa vifaa huku ukipunguza uwezekano hatarishi wa zana kupotea katika mifumo muhimu ya ndege wakati wa matengenezo.
Mfumo huo ukiwa umeunganishwa na kituo kikuu cha mawasiliano kupitia njia ya mtandao na hivyo kuuwezesha kukagua zaidi ya matengenezo 15,000 yaliyofanyika, mfumo huu utaweza kutambua vifaa vilivyo potea, kuvunjika au vilive ambavyo havijarudishwa.
Mkebe wa vifaa hautoweza kufunguliwa mpaka mhandisi aonyeshe kitambulisho chake mbele ya kifaa maalumu ha kuhakiki kilichopo mbele ya mkebe huo wa vifaa. Kitambulisho kitasaidia kuhakikisha mhandisi anamamlaka ya kutumia vifaa ndani ya mkebe husuika na hivyo mkebe kufunguka. Mkebe huu wa vifaa unakuja na sehemu ya mhandisi kujaza matengenezo anayotakiwa kufanya (Idadi/Aina) pamoja na eneo la kazi.
Mfumo huu mpya ulipitia majaribio yenye mafanikio katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Abu Dhabi mnamo mwezi Novemba mwaka 2015, na ulikwisha sambazwa katika vituo vyote vya shirika la ndege la Etihad vya matengenezo mwezi Januari.
Karibu wafanyakazi 350 wamepata mafunzo juu ya mfumo mpya, na zaidi ya matengenezo 50,000 yamekwisha fanyika bila upotevu wa kifaa chochote cha ufundi.
Jeff Wilkinson, Makamu wa Rais, Etihad Airways, Ufundi, alisema: "Udhibiti wa vifaa ni swala muhimu kwa ajili ya mafanikio hasa pale tunapolenga kuboresha shughuli ya matengenezo ili kupunguza michakato ya kazi, kuongeza ufanisi na kuimarisha usalama.
"Kupitia mfumo mpya, wahandisi wetu ni wataweza kumaliza matengenezo haraka na kwa ufanisi, bila ya kuchukua hatua za ziada kufuatilia, kujiandikisha au kuangalia walipoacha vifaa wanavyotumia na hivyo kuokoa kwa kiasi kikubwa muda."
"Hii pia huongeza usalama kwani kifaa kilichopotea mikononi mwa mhandisi sio tu usumbufu bali kinageuka kuwa kifaa hatarishi kwa usalama wa mtu mwingine" aliongeza
Mfumo huu unawezesha mikebe yenye vifaa hadi 1,000 mbalimbali ndani yake pamoja mikebe mingine yenye na vifaa maalumu kwa ajili ya matengenezo ya umeme na uhandisi wa ndani ya ndege, kupangiwa mhandisi mwenye mamlaka husika aliyepangiwa kazi maalumu kwenye dege.
Kitengo cha uhandisi wa matengenezo ya ndege cha Shirika la Ndege la Etihad hivi sasa kina mikebe 32 ya vifaa vya matengenezo vinavyotumia mfumo huu mpya ndani yake, kati yake mikebe isiyopungua 20 huwa inatumika kwa wakati mmoja. Mifumo iliyobaki itaunganishwa na kituo kikuu na hivyo kuwezesha mifumo hiyo kama inavyotakiwa ili kukidhi mahitaji ya timu matengenezo kama ndege inakuja katika kwa ajili ya matengenezo.