Wednesday, March 30, 2016

GNAKO AZUNGUMZIA HASARA WALIYOPATA BAADA YA DIRECTOR NISHER KUVUJISHA AROSTO



GNAKO AZUNGUMZIA HASARA WALIYOPATA BAADA YA DIRECTOR NISHER KUVUJISHA AROSTO

Ni hivi Majuzi Director Nisher alivujisha Kipande cha Video ya Wimbo wa GNako na Nikki Wa Pili Arosto Kitu ambacho Wasanii hao Kutoka Kundi la Weusi Waliki Mind Sana.
Utakuwa na Kumbukumbu kwamba GNako na Nikki wa Pili walikuja Arusha na Kuweka Kambi Kushuti Kile Walichokiita kuwa ni Movie yao ya Pamoja ambayo inakwenda kwa jina la Arosto ila Baadae Nisher alichokipost Bila Idhini yao ni Kipande cha Video ya Wimbo wao wa Arosto Sasa Tumemtafuta GNako atupe Majibu Kwamba Movie Hiyo Imeishia Wapi na Je Ni Movie au ni Wimbo Tu alakini ni Hasara Ipi Wameingia baada ya Director Huyo Kuvjisha Kipande Hicho cha Video.
Kwenye Majibu ya Movie Imeishia wapi GNako amesema Kila Kitu kinaenda Poa Ila Bado Muda wa Kutoka haujafika na Hiyo Clip Iliyosambaa ni Sample Tu ila Movie yenyewe ya Arosto Haijatoka.
Jibu la Pili ni kuhusu Tetesi za Kuwepo Beef Kubwa kati yao na Director Nisher na Amejibu kwamba Hakuna Shida yoyote kati yao Isipokuwa Wameichukulia tu kama Hitilafu iliyotokea katika Kazi Hivyo Wao Hawana Shida.
Jibu la Tatu Linahusu Hasara wanayohisi Wamepata baada ya Kuvuja Huko kwa Kipande hicho cha clip bila Idhini yao na Majibu yake amesema Sio Shida sana kwani watu bado wanaham ya Kupewa Kitu Kamili kwahiyo kwa Upande wake sio Kitu Kikubwa sana.
Kuhusu Wasiwasi wa Kwamba Arosto ni Ngoma au ni Movie GNako amesema Watu wasikilizie tu na Soon watapata Kujua kama ni Movie au ni ngoma.