Monday, December 21, 2015

BOMOA BOMOA KUPINGWA MAHAKAMANI


BOMOA BOMOA KUPINGWA MAHAKAMANI
 

Mtulia alitangaza dhamira yake hiyo jana alipowatembelea wakazi wa Mkwajuni waliokumbwa na bomoabomoa hiyo.


Akiwa katika eneo hilo, Mtulia alielezwa na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Hananasif, Deogratius Mogela kwamba kati ya wakazi 375 wa mtaa huo ambao nyumba zao ziliwekewa alama kwa ajili ya kupewa viwanja, ni 21 tu ndiyo waliokabidhiwa.
"Wengine tuliambiwa tusubiri awamu nyingine, lakini tumeshangaa nyumba zetu zote zimebomolewa wakati ahadi bado haijatekelezwa," alidai Mogela.
Akifafanua mbunge huyo, alisema anataka ubomoaji huo usimame mpaka ufumbuzi wa tatizo hilo la viwanja utakapopatikana.
"Manispaa ya Kinondoni na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi tukae pamoja tufanye tathmini ili walionufaika na viwanja vya Mabwepande wajulikane, inaonekana viwanja hivi vimekwenda kwa watu wasio walengwa," alisema.
Mtulia alisema hatetei watu wanaoishi kwenye maeneo hatarishi, bali wanapaswa kupatiwa viwanja ndipo wahame.
Bomoabomoa hiyo itaendelea tena leo katika eneo la Hananasif.

MWANANCHI.