Thursday, December 03, 2015

Balozi Mero ashiriki Mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda Duniani (UNIDO) unaofanyika Vienna, Austria



Balozi Mero ashiriki Mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda Duniani (UNIDO) unaofanyika Vienna, Austria
Balozi Modest Jonathan Mero, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataiafa na Mashirika mengine ya Kimataifa Geneva na Vienna akiwasilisha hotuba ya Tanazania katika mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda Duniani ambao unajadili maendeleo endelevu ya viwanda kama njia mbadala ya kuzikwamua nchi maskini. Mkutano huu unafanyika jijini Vienna, Austria kuanzia tarehe 30 Novemba hadi tarehe 4 Desemba 2015.

Katika hotuba yake, Mhe. Balozi Mero, pamoja na mambo mengine aliwaleza wajumbe wa mkutano huo hatua mbali mbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kukuza viwanda nchini ikiwa ni pamoja na mafanikio ambayo yamefikiwa hadi sasa.

Mhe. Balozi Mero pia alizungumzia juu ya mapitio ya Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo wa awamu ya pili (National Development Plan Phase Two) ambao utatekelezwa na Serikali kuanzia 2016/2017 hadi 2020/2021 ambao pamoja na mambo mengine umeweka msisitizo wa kukuza viwanda kwa lengo la kuongeza thamani ya rasimali zetu, kukuza mahitaji ya ndani ya bidhaa za viwandani na kuongeza ajira kupitia viwanda, Sekta nyingine za uzalishaji, huduma duniani.