Monday, November 16, 2015

WATANO WAOKOLEWA KATIKA MGODI WA NYANGARATA KAHAMA.


WATANO WAOKOLEWA KATIKA MGODI WA NYANGARATA KAHAMA.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WATU watano wamepatikana wakiwa hai tangu Oktoba 5 mwaka huu walipofukiwa na kifusi cha mchanga katika mgodi wa wachimba wadogo wa mgodi wa Nyangarata wilaya ya Kahama  mkoani Shinyanga, watu hao waligundulika kuwepo ndani ya mgodi hou mita 100 kwenda chini ikiwa mtu mmoja amegundurika kuwa amefariki dunia.

Waliookolewa katika  mgodi huo kuwa ni Josef Burule, Chacha Wambura, Msafiri Gerald, Onyiwa Aindo na Amosi Mhangwa pia limtaja aliyefariki dunia ni Mussa Supana.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Massoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. 

amesema kuwa watu hao wamekaa chini ya ardhi kwa zaidi ya siku 40 ambapo mgodi huo ulianza kudidimia kwenda chini, Oktoba 5 mwaka huu mpaka Novemba  15 ambapo waokoaji kutioka Wizara ya Nishati na Madini walianza kuwatafuta ndipo jana wakafanyikiwa kuwatoa wakiwa na hali mbaya na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Pia amesema kuwa walipokuwa chini huko wakuwa wanakula magome ya miti pamoja na maji walikuwa wanakinga  yaliyokua yakitililika kidogo na kukinga katika helementi zao ambazo walikuwa wamezivaa walipokuwa wanaingia katika mgodi huo.

Pia Badra alitoa wito kwa wachimbaji wadogo wa Madini kuwa wachimbe kwa kutumia vifaa vya kisasa ili kuepukana na madara yoyote yatakayo jitokeza katika uchimbaji wa madini.
 Afisa habari wa Wizara ya nishati na Madini, Badra Massoud akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana na watu waliopatikana wakiwa hai katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa Nyangarata mkoanI Kahama.
Afisa habari wa Wizara ya nishati na Madini, Badra Massoud akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Kulia ni Afisa habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Jaiquline  Mrisho.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.