Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limesema bado taratibu za kuwatambua wahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha na kupotea kwenye wakati wa ibada ya Hijja kwenye mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia katika tukio la kukanyagana na kusababisha watu 717 kupoteza maisha zinaendelea kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Bakwata, Suleman Said Lolila, alisema Watanzania ambao wamethibitishwa kufariki dunia bado ni walewale wanne wakati taarifa zaidi zikisubiriwa kuhusiana na tukio hilo.
"Kuna Wanzania waliopotea na hawajaonekana hadi sasa na tunaendelea kuwatafuta na waliopotea si wao tu bali pia wapo mahujaji kutoka mbalimbali, hivyo tusibiri," alisema Lolila.
Takribani mahujaji 717 walipoteza maisha katika tukio hilo wakiwamo Watanzania wanne na raia wa Kenya mmoja ambaye alikuwa akiishi nchini.