Wednesday, September 23, 2015

AKAMATWA KWA KUHIFADHI SEHEMU ZA SIRI


AKAMATWA KWA KUHIFADHI SEHEMU ZA SIRI
Image captionPeter Fredekrisen alikamatwa na maafisa wa polisi wa Afrika Kusini kwa kuhifadhi sehemeu za siri za wanawake 21 katika jokovu
Maafisa wa polisi nchini Afrika Kusini wameomba kupewahabari zaidi baada ya kumkamata raia mmoja wa Denmark kwa madai ya kuhifadhi sehemu za siri za wanawake 21 katika jokovu.


Peter Fredekrisen,ambaye anamiliki maduka mawili ya bunduki mjini Bloemfontein anakabiliwa na mashtaka ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,vitisho na unyanyasaji wa majumbani.
Raia huyo wa miaka 58 anadaiwa kuwapatia dawa za kulala waathiriwa kabla ya kuwafanyia upasuaji.
Bwana Fredekrisen hakutakiwa kujibu mashtaka wakati wa kusikizwa kwa kesi yake siku ya jumatatu.
Brigedia Hangwani Mulaudzi kutoka katika kitengo cha upelelezi nchini Afrika Kusini ameiambia BBC kwamba mshukiwa huyo atasalia mahakamani hadi atakaporuhusiwa kuomba dhamana. Jumatatu ijayo.
Polisi wanaamini kwamba wateja wake walikuwa wakitoka katika eneo jirani la Lesotho.
Mwandishi wa BBC Milton Nkosi mjini Johannesburg amesema kuwa bwana Fredekrisen alikamatwa wiki iliopita kufuatia habari.
Sehemu hizo za siri zilipatikana katika jokovu ,zikiwa na majina ya wanawake waliotolewa na kule wanawake hao walikotoka.
Dawa za kulevya na vifaa vya upasuaji vya madaktari pia vilipatikana katika nyumba yake,polisi wanasema.