Eneo la kibiashara la Kariakoo jijini Dar es Salaam ni mfano hai wa jinsi watu wa mataifa ya nje, zaidi ya Wachina, ambao wanafanya biashara za kawaida kama vile maduka madogo ya kawaida ambayo yanamilikiwa na Watanzania wa kawaida wenye mitaji midogo.
Swali ambalo Watanzania wanajiuliza ni kwamba wageni hawa 'Machinga' ni wawekezaji au ni watu waliokwepa macho ya serikali na kuingia mitaani kuwazibia riziki Watanzania! Kama wanafanya hivyo kinyemela, ni nani hasa mwenye mamlaka ya kuweza kuwaondoa mitaani na kuhakikisha 'uwekezaji' wa aina hii unaondoka mitaani?
CHANZO: BBC SWAHILI