Wafanyabiashara wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na serikali wamezisaidia chakula, vifaa vya ujenzi pamoja na fedha kaya kumi na sita zilizokuwa zikilala nje baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo katika kata ya matarawe mkoani humo.
Mwenyekiti wa jumiya ya wafanyabiashara mkoa wa Ruvuma Bw. Tito Mbilinyi amemkabidhi katibu tawala wa wilaya ya songea Bw.Ally Juma vifaa hivyo vikiwa na thamani ya shilingi 1992,000 ikiwa pamoja na pesa huku serikali ikiwa imechangia s hilingi 885,000 na kufanya jumla ya pesa zote kuwa milioni mbili elfu themanini na sabini na tano ili awakabidhi wahanga wa maafa yaliyotokea aprili tano na kuziacha kaya kumi na sita zikilala nje.
Katibu tawala huyo ameshukuru kwa mchango huo wa wafanyabiashara.
Nao wananchi waliokumbwa na maafa hayo matarawe songea aprili tano siku ya pasaka wameshukuru kwa msada huo kwa kuwa walikuwa wanalalaa nje.