Saturday, April 25, 2015

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AZINDUA KITABU CHA KIHISTORIA



NAIBU WAZIRI WA FEDHA AZINDUA KITABU CHA KIHISTORIA
Mwandishi wa kitabu cha kihistoria na Mhariri Mkuu, Simai Mohammed Said akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Mchapishaji wa kitabu hicho, Javed Jafferji akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Adam Kighoma Malima akizungumza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa fedha na Uchumi, Adam Malima(katikati) akionesha ishara ya Uzinduzi wa kitabu hicho sambamba na mwandishi wa kitabu hicho (kulia) pamoja na mchapishaji wa kitabu hicho(kushoto).
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul akisalimiana na Naibu Waziri wa fedha katika uzinduzi huo.
Nasib Abdul 'Diamond' tayari akiwa amekabidhiwa kitabu cha kihistoria kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima katika hafla hiyo.Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo.
NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi, Adam Kighoma Malima  amezindua kitabu cha kihistoria kiitwacho Photographic Journey 50 years of The United Republic of Tanzania kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa awe mgeni rasmi, uliofanyika katika mojawapo ya kumbi zilizopo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Kitabu hicho chenye kurasa 444 kilichotungwa na Simai Mohamed, kinazungumzia mambo mbalimbali ya historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuthamini michango ya wasanii mbalimbali nchini na Naibu Waziri Malima, alichukua fursa hiyo kumpongeza kwa mambo aliyoandika na ubunifu wa hali ya juu uliomo ndani yake.
Aidha, katika kitabu hicho kuna mambo mbalimbali ya kukumbukwa ikiwa ni pamoja na kupanda mlima Kilimanjaro, vita vya Kagera na vivutio vya kitalii Tanzania.Msanii mwalikwa, Nasib Abdul 'Diamond' alikabidhiwa nakala ya kitabu hicho ambacho mojawapo ya kurasa zake za ndani, zinamzungumzia.
(PICHA/ STORI:DENIS MTIMA NA MUSA MATEJA / GPL)