Tuesday, April 28, 2015

BI BETTY MKWASA AHAMASISHA UJENZI WA MAABARA DODOMA MJINI


BI BETTY MKWASA AHAMASISHA UJENZI WA MAABARA DODOMA MJINI

MKUU  wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bi. Betty Mkwasa amekuwa kwenye kampeni ya kuhamasisha ujenzi wa vyumba vya maabara katika Wilaya yake, ikiwemo kushiriki mwenyewe katika kazi za ujenzi wa vyumba hivyo. Katika harakati hizo Bi Mkwasa alikutwa akishirikiana na umoja wa wasanii wa Dodoma , Dodoma All Stars wakishiriki katika ujenzi wa chumba cha maabara katika kijiji cha Mkonze. Pamoja na mengi mengine kutakuwa na tamasha kubwa la muziki kuhamasisha ujenzi wa vyumba vya maabara katika wilaya hiyo ambapo tarehe 2 Mei 2015, katika uwanja wa Jamhuri Stadium, wasanii kama Ben Pol, Bushoke, Mzee Yusuph watapanda jukwaani pia wakishirikiana na wasanii wengine wa Dodoma wanaoishi Dodoma na wale wanaoishi nje ya  Dodoma. Kiingilio katika onyesho hilo litakuwa 3000/- kwa watoto na 5000/- kwa wakubwa. Usiku raha zitahamia Royal Village ambapo mambo yataanza saa 4 usiku na kuendelea hadi majogoo. Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

IMG-20150425-WA0252 IMG-20150425-WA0253 IMG-20150425-WA0255 IMG-20150425-WA0256#1 IMG-20150425-WA0257 IMG-20150425-WA0258 IMG-20150425-WA0259