Monday, March 09, 2015

Wafanyakazi Wa Kiwanda Cha Sukari Mtibwa Wagoma Kufanya Kazi Na Kufunga Njia


Wafanyakazi Wa Kiwanda Cha Sukari Mtibwa Wagoma Kufanya Kazi Na Kufunga Njia

Wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa wilayani Mvomero mkoani Morogoro wagoma kufanya kazi na kufunga njia inayo ingia katika kiwanda  hicho kushinikizau ongozi wa kiwanda kuwalipa mishahara yao ya miezi miwili.

Wakizungumza kwa uchungu huku wakionekana wakipika ugali katika ofisi kuu ya kiwanda cha sukari cha mtibwa wananchi hao wamesema wataendelea kupiga kambi katika kiwanda hicho hadi watakapolipwa mishahara yao kwani wanashindwa kuendesha maisha ya familia zao huku wengine wakilalamikia kushindhwa kuwalipia watoto wao ada mashuleni na kusababisha  waanafunzi kushindwa kuendelea na masomo kwa kurudishwa nyumbani.

Diwani wa kata ya mtibwa Lucas Mwakambaya amesema yupo tayari kuwaunga mkono wananchi hoa kudai haki zao kwani hali ya maisha ya  wananchi wake ni mbaya ambapo amesema kama uongozi wa kiwanda haupotayari kuwalipa kwa hiyari basi watawalipa kwanguvu kwani madai hayo ni ya msingi na nihaki ya kila mfanyakazi kulipwa madaiyake.

Meneja wa kiwanda cha sukari mtibwa Ahimerd Yahaya alipo tafutwa na kuzungumzia malalamiko ya wafanyakazi hao hakuweza kupatika na simu zake zilikuwa zikiita tu  mgomo huo ni wapili kutokea hivi karibuni wakulima wa miwa turiani nao waliandamana wakilalamikia kiwanda cha miwa mtibwa kushindwa kuwalipa.