Thursday, March 12, 2015

IGP Mangu apeleka makachero katika sakata la watoto 18 waliokuwa wamepotea mkoani Kilimanjaro.


IGP Mangu apeleka makachero katika sakata la watoto 18 waliokuwa wamepotea mkoani Kilimanjaro.
Siku chache baada ya kugundulika mahali walipofichwa watoto 18 ambao wamepotea katika mazingira ya kutatanisha kutoka mikoa nane hapa nchini  mkuu wa jeshi la polisi nchini  IGP Ernest Mangu amekutana kwa saa kadhaa na maafisa wa jeshi hilo mkoani Kilimanjaro.




Hatua ya IGP Mangu imekuja baada ya jehi hilo kutuma kikosi maalumu cha makachero kutoka makao makuu ya polisi kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi cha uchunguzi wa tukio hilo.

Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilaya ya Moshi Bw.Novatus Makunga amesema tayari kikosi hicho kimeshaanza kazi na kwamba hadi sasa uchunguzi wa awali umebaini uwepo wa kituo kingine kama hicho maeneo ya kibosho mwisho wa daladala.
Katika hatua nyingine Bw.Makunga amesema tayari watoto hao wamesharejeshwa kwa wazazi wao baada ya wananchi waliojitokeza kukidhi vigezo vya mashariti vilivyowekwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Moshi.
Wakili wa mahakamu kuu ya Tanzania, kanda ya Moshi na mwenyekiti wa mwavuli wa asasi za kiraia mkoa wa Kilimanjaro, Bi Elizabeth Minde amesema wamepokea tukio hilo kwa masikitiko makubwa, kwa kuwa linaweza likawa na sura tofauti ikiwamo kuhusishwa na biashara ya binadamu. 
Tukio la kupatikana kwa watoto hao wenye umri kuanzia miaka miwili hadi 16 liligundiliwa machi 7, mwaka huu katika nyumba ya mfanyabiashara wa nguo, nchini Kenya, Bw. Abdelinasir Abdurahamni; ambapo watoto hao wametambuliwa wanatokea mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Arusha, Kagera, Mara, Dodoma na Shinyanga.

CHANZO: ITV