Tuesday, February 03, 2015

Wananchi Monduli wafunga njia za minara ya simu


Wananchi Monduli wafunga njia za minara ya simu


Wananchi  kijiji cha  Losimingori   wilayani   Monduli  mkoani  Arusha  wamefunga   kwa  muda  barabara  zote  zinazokwenda  kwenye   minara  ya  mawasiliano  ya  simu  za  mkononi wakizidai kampuni  hizo   zaidi  ya  bilion  moja  yakiwa  ni  malimbikizo  ya  kodi  ya  miaka  nane   sasa.

Wakizungumza kwa jazba katika mkutano wa  kutafuta  muafaka   wa  sakata  hilo  ,wananchi  hao wamesema wamefikia  hatua  hiyo  baada ya kubaini  kuwa  viongozi  wao  wa  vijiji  wamekuwa  wakikwepa  kuwaeleza  ukweli  wa  fedha  zao .\

Hata hivyo   baada  ya  mvutano mkali  baadhi  ya viongozi  wa  kijiji  hicho  walifanikiwa  kuwatuliza  wananchi hao  na  kufungua  barabara  hiyo   huku  wakitoa  siku tatu   za  kupatiwa  majibu   ya  kueleweka  kabla  hawajachukua  hatua  nyingine 

Wakizungumzia  sakata  hilo   wawakilishi   wa  makampuni hayo  akiweamo   mhandisi  Regan  Usiri  pamoja  na  kuwaomba  wananchi  hao  kuwa  na subira  ili  wakati   wanafuatilia   madai  yao    wamesema   wanachojua  wao   ni  kwamba   fedha  hizo   zimelipwa  kwa  taasisi  ya  jeshi   la  wananchi  kwa  madai  kuwa  ndiyo  wanaomiliki  eneo   iliko  minara  hiyo  maelezo ambayo yamepingwa  vikali  na  wananchi  hao .

Pamoja  na  mkanganyiko huo   viongozi  wa  vijiji  wameahidi  kufuatilia  suala  hilo  ngazi za  juu  na ili  kujua  ukweli   na  kumaliza  utata  huo  ambao  ulisababisha  baadhi ya  huduma  kwenye  minara hiyo   kusimama