Jeshi la wananchi nchini (JWTZ) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini limeahidi kukabiliana na makundi ya watu wanaodaiwa kuwa majambazi sugu ambao wanapora silaha za askari huku wengine wakiuawa hatua ambayo imeanza kutishia usalama wa nchi.
Akizungumza na jijini tanga kufuatia hivi karibuni makundi hayo kupora silaha na kisha kuua askari huko rufiji mkoani pwani na wengine wakipora askari wawili silaha nyakati za usiku jijini tanga na kisha kuwadhuru hatua ambayo imesababisha kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga bombo,katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa JOB MASIMA amesema vyombo vya ulinzi vitakaa na kuhakikisha kuwa mtandao huu unapatikana ili kurejesha silaha hizo.
Hata hivyo katibu mkuu amekana vikali kuwa huenda makundi haya ya uhalifu yanayojihusisha na kupora silaha askari kwa na wahitimu waliopitia mafunzo ya jeshi la kujenga taifa JKT ambao baadhi yao hawakupata ajira baada ya kurudu uraiani na kuongeza kuwa hata wanaojihusisha na ugaidi sio wote ambao wamepitia mafunzo ya kijeshi.