Saturday, January 03, 2015

MAJENGO YABOMOKA MENGINE HATARINI KUWAANGUKIA WATOTO,MH. RIDHIWANI ASIKITISHWA


MAJENGO YABOMOKA MENGINE HATARINI KUWAANGUKIA WATOTO,MH. RIDHIWANI ASIKITISHWA
Na John Gagarini, Kibindu

WANAFUNZI wa shule ya Msingi Kibindu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wako hatarini kuangukiwa na vyumba vya madarasa wanayosomea kutokana na ubovu wa vyumba hivyo ambavyo vimejengwa miaka ya 50.

Mwishoni mwa mwaka jana vyumba vya madarasa mawili na ofisi ya mwalimu vilianguka na kuezua mapaa ya vyumba vine vya madarasa na ofisi ya mwalimu mkuu baada ya kutokea mvua kubwa amabyo iliambatana na kimbunga.

Shule hiyo ambayo ina wanafunzi 970 hawakuwepo shuleni kwani walikuwa wako likizo ya mwisho wa mwaka baada ya shule kufungwa mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye alitembelea shuel hiyo ofisa mtendaji wa kijiji cha kibindu Juma Athuman alisema kuwa mvua hiyo kubwa iliambatana na kimbunga ilinyesha Desemba 28 mwaka jana  na kuangusha majengo mawili ya madarasa pamojana na kueezua mapaa ya vyumba  vinne vya madasa na  na ofisi ya mwalimu mkuu.

Athuman alisema kuwa kimunga hicho pia kilisababisha ufa katika majengo mengine kadhaa ya madarasa katika shule hiyo na  kuwa katika hatari kubwa ya kuanguka.

"Hali hiyo inatia wasiwasi kwa wanafunzi wnaotarajiwa  kuanza  masomo Januari  14 mwezi huu kuwa hatarini kuangukiwa na majengo hayo endapo hatua za dharura hazitachukuliwa," alisema Athuman.

Akizungumzia  mara  baada ya kutembelea shule hiyo  Mbunge wa Jimbo la Chalizne Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na hali hiyo ya majengo ya shule hiyo  na kusema kuwa anafanya taratibu za kuwasiliana na mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kuona jinsi ya kujenga upya shule hiyo.
Diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya aliyenyanyua mikono juu akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kulia aliyevaa kofia ya kijani kufuatia mvua kubwa kubomoa madarasa ya shule ya Msingi Kibindu.
Moja ya madarasa ya shule ya msingi Kibindu likiwa limebomoka kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa mwaka jana.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa Habari mbele ya jengo la shule ya Msingi Kibindu ambalo lilianguka kufuatia mvua kubwa ziulizonyesha mwishoni mwa mwaka jana kushoto ni diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza wananchi wa Kata ya Kibindu alipofika kuwajulia hali kufuatia mvua kubwa ziulizonyesha mwishoni mwa mwaka jana.