Naibu Mkurugenzi wa Habari wa Bank M,Allan Msalilwa akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Hayyat Regency ,jijini Dar es Salaam juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu Biashara wa Bank M,Jacqueline Woiso akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uboreshaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.
======= ======== ======== ===========
Na Chalila Kibuda na Globu ya Jamii,Dar.
Benki M imesema imeendelea kuboresha huduma kwa wateja katika uendelezaji wa viwanda pamoja na mikopo katika miradi ya jamii ikiwepo kudhamini maji.
Akizungumza na waandishi leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Hayyat Regency Jijini Dar es Salaam,Afisa Mtendaji Mkuu wa Biashara wa Benki M,Jacqueline Woiso ,alisema kufanya hivyo kuboresha hivyo ni kutaka wateja wa benki M kuendelea kunufaika.
Alisema mikopo waliositisha ni ya nyumba pamoja na elimu na kufungua milango ya mikopo kwa taasisi kwa ajili ya maji na viwanda ili kuweza wananchi kunufaika katika viwanda pamoja na maji.
Jacqueline alisema benki inawakaribisha wateja wapya kujiunga na benki hiyo ili kuweza kunufaika na huduma mpya zitakazoweza kusaidia jamii kupata maendeleleo.
Aidha alisema huduma nyingine ni uwekaji wa mashine ya kukusanyia fedha kutoka kwa wateja ili kuondoa usumbufu kutoka sehemu moja kwenda nyingine