Wednesday, December 03, 2014

WANABIAFRA WASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA KUHAMASISHA MICHEZO KWA VIJANA NA WATOTO



WANABIAFRA WASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA KUHAMASISHA MICHEZO KWA VIJANA NA WATOTO
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) chini ya udhamini wa taasisi ya UK Sports - Internationa Inspiration iliandaa mafunzo uhamasishaji wa michezo kwa vijana na watoto. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika uwanja wa taifa yaliwakutanisha pamoja makatibu tawala pamoja na maafisa michezo toka katika wilaya zote nchini. Mafunzo hayo pia yalifanyika ikiwa ni sehemu ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wa baraza la Michezo Tanzania uliofanyika katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Mkinga, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Makatibu Wakuu na Wenyeviti wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. (picha kwa hisani ya Hivi Sasa Blog).
Baada ya mafunzo hayo, sherehe  rasmi ya uzinduzi wa kampeni ya Inspire Tanzania ilifanyika tarehe 20 September, 2014 katika uwanja wa taifa. Sherehe hiyo ilitanguliwa na mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambayo yaliratibiwa na klabu ya michezo ya Biafra pamoja na vilabu vingine vya jogging katika mkoa wa Dar es Salaam ambavyo Temeke Jogging, Faita, Jogging, Kopa Jogging, n.k.