Wednesday, December 17, 2014

SERIKALI YAWASIMAMISHA WAKURUGENZI WALIOSHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA



SERIKALI YAWASIMAMISHA WAKURUGENZI WALIOSHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
      Na Bakari Issa,Dar es Salaam

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI leo imetangaza kuwasimamisha kazi Wakurugenzi watano (5) huku wengine wakipewa onyo kali katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akithibitisha kusimamishwa kazi kwa Wakurugenzi hao,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Mh. Hawa Ghasia amesema kwamba Wakurugenzi hao wametenda makosa yanayowaondolea sifa za kuwa Wakurugenzi.

"Makosa yafuatayo ndio yanayopelekea Wakurugenzi hawa kusimamishwa;Kuchelewa kuandaa vifaa vya kupiga kura,kukosa umakini katika kuandaa vifaa hasa karatasi za kupigia kura,kuchelewa kupeleka vifaa kwenye vituo vya kupigia kura,uzembe katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maandalizi ya uchaguzi kuwa yamekamilika huku wakijua kuwa siyo kweli",alisema Ghasia

Aidha,Mh.Ghasia ameridhishwa na hatua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumchukulia hatua mtumishi wake aliyemsingizia Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali na kusema ni jambo baya kutenda kosa na kusingizia watu au ofisi zisizohusika.

Wakurugenzi wanaosimamishwa kazi na kupisha uchunguzi zaidi ni pamoja na

i)                    Bw.Felix T.Mabula-Halmashauri ya Hanang'
ii)                  Bw.Fortunatus Fwema- Halmashauri ya  Mbulu
iii)                Bi.Isabela D.Chilumba- Halmashauri ya  Ulanga
iv)                Bi.Pendo Malabeja- Halmashauri ya  Kwimba
v)                  Bw.William Z.Shimweta-Sumbawanga Manispaa

Pia, Mh.Hawa  Ghasia amesema Wakurugenzi wengine watatu(3) wanapewa onyo kali na watakuwa chini ya uangalizi kubaini kama wana udhaifu mwingine ili wachukuliwe hatua zaidi Wakurugenzi hao ni:-

i)                    Bw.Mohamed  A.Maje-Halmashauri ya Rombo
ii)                  Bw.Hamis Yuna- Halmashauri ya Busege
iii)                Bw.Jovin A.Jungu- Halmashauri ya Muheza