Napenda kupitia blog hii ya jamii kuwakaribisha watu wote katika jiji hili la Dallas,Texas katika semina kubwa ya neno la Mungu itakayofanyika katika jiji letu. Mtumishi wa Mungu anaeheshimika ndani na nje ya nchi yetu Dr.Daniel Moses Kulola ndie atakae tuhudumia.
Daniel Kulola ni mtoto wa marehemu mzee Moses Kulola,mtumishi ambae ametoa mchango mkubwa sana wa injili katika Taifa letu kabla hajaenda kukaa na Bwana. Ili kuhakikisha kila mtu anapata nafasi ya kuhudhuria semina hii; kanisa lako la Umoja limetoa basi maalumu litakalo wahudumia watu wote ambao wanahitaji usafiri. Dr. Daniel pichani atatuhudumia siku siku zifuatazo;
Ijumaa kuanzia 12 jioni -2 jioni (6:00 Pm-8:00Pm)
Jumamosi Kuanzia 10 jioni-12:30 Jioni (4:00Pm-6:30Pm)
Jumapili kuanzia 11:30 jioni- 2 jioni (5:30 Pm-8:00 Pm)
Tunaomba kila moja wetu azingatie muda haswa siku ya Jumamosi kwani ndio jumuia yetu inasherekea siku ya uhuru wa Taifa letu.
Anuani: Umoja International Outreach Church
6411 LBJ Freeway,Dallas Texas,75240
Simu: 214 554 7381, 682 552 6402
Pastor Absalom Nasuwa