Wednesday, December 03, 2014

Sasa NMB kuwafikia wateja wake Mpaka Vijijini kupitia NMB Wakala



Sasa NMB kuwafikia wateja wake Mpaka Vijijini kupitia NMB Wakala
Banki ya NMB imeingia makubaliano na kampuni ya Maxcom kupitia mtandao wa mawakala wanaojulikana kama Max Malipo kwaajili ya kuanza kutoa huduma za kibenki. HUduma hii itakuwa inaitwa NMB Wakala na itakuwepo kwenye kila wakala wa MaxMalipo waliotapakaa nchi nzima.

Kuingia kwa MaxCom kwenye benki ya NMB kunamaanisha kuwa NMB itazidi kupanua Zaidi mtandao wao kwa kuingia hadi vijijini tofauti na benki zingine. Kupitia mawakala wa MaxCom, wateja wa NMB wanaweza kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti zao za NMB, kuangalia salio, kulipia huduma mbalimbali na hata kutuma fedha.

Kwa sasa NMB ndiyo benki yenye mtandao mpana Zaidi kwani wana matawi Zaidi ya 160 na mashine za ATM Zaidi ya 500. 

Ujio wa MaxCom ni dhahiri kabisa kuwa NMB imedhamiria kwenye tekinolojia kwani mpaka sasa, mbali ya matawi yao mengi, bado wanatumia huduma nyingine kama Mpesa, Tigo Pesa, NMB Mobile, Pesa Fasta na zinginezo nyingi zinazolenga kusogeza huduma karibu Zaidi ya wateja wao.
Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya NMB Mark Wiessing (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom Africa Bw. Juma Rajabu wakibadilishana Mkataba waliousaini ikiwa ni makubaliano ya Mteja yeyote wa NMB anaweza kupata Huduma za kibenki kwa wakala wa Maxcom popote nchini. Hafla hii adhimu ilifanyika jijini Dar es salaam.
Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya NMB (kulia) Mark Wiessing na Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom Africa -Juma Rajabu wakiweka Sahihi kwenye Mkataba ikiwa ni makubaliano ya Mteja yeyote wa NMB anaweza kupata Huduma za kibenki kwa wakala wa Maxcom popote nchini. Hafla hii adhimu ilifanyika jijini Dar es salaam.
Mkuu wa kitengo cha Huduma Mbadala cha NMB George Kivaria akifafanua kuhusu makubaliano ambayo NMB imeingia na kampuni ya MaxCom. Pembeni ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MaxCom Africa Bwana Juma Rajabu.