Wapiganaji wa Islamic State katika jimbo la Anbar,Syria Marchi 2014
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo LibyaWapiganaji wa kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika.
Wapiganaji wa Kikurd wakiwa katika mafunzo ya kijeshi kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State Septemba 2014 nchini Iraq.Jenerali David Rodriguez amesema kuna mamia ya wapiganaji wa IS wanaopata mafunzo ya kijeshi kwenye kambi zake nchini Libya. Amesema kambi hizo zipo katika hatua za mwanzo kabisa, lakini Marekani imekuwa ikiyafuatilia kwa karibu kuona zinavyoendelezwa.
Libya imekuwa katika mgogoro tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, ambapo makabila mbalimbali, wanamgambo na makundi ya kisiasa, wote wakipigania madaraka.
Makundi mbalimbali ya Kiislam yanawania madaraka mashariki mwa Libya, hukubaadhi yakitangaza kuwa na ushirikiano la kundi la Islamic State, IS.
Wapiganaji kutoka kikundi cha IS wakipakia mabaki ya kile kinachosemekana kuwa mabaki ya ndege ya Marekani isiyotumia abiria baada ya kukonga katika mnara wa mawasiliano huko Raqqa Septemba 23,2014Akizungumza mjini Washington Jumatano, Jenerali Rodriguez bado haijafahamika ukaribu uliopo kati ya watu wanaopata mafunzo hayo na kundi la IS."Kikubwa ni watu wanaokuja kupata mafunzo na msaada wa vifaa kwa ajili ya kambi za mafunzo kwa sasa," amesema. "kwa sasa mafunzo hayo bado ni ya hatua ya chini sana na tunafuatilia kuona namna hali inavyokwenda."
Watoto wakikimbia kando ya mlima hukumoshi ukisambaa angani kufuatia mapigano katika eneo hilo la mji wa Kobani, wakati majeshi yanayoongozwa na Marekani kushambulia wapiganaji wa Islamic StateWaandishi wa habari wanasema katika kipindi cha mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Gaddafi, wapiganaji wengi waasi waliondoka nchini humo kwenda kujiunga na vikundi vya wapiganaji nchini Syria na baadhi yao wanaaminika kuwa wamerejea nyumbani(Libya).
Serikali iliyochaguliwa imepoteza miji mikuu mitatu ya Libya huku kukiwa na mgogoro wa kisiasa.
Benghazi, mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya, uko mikononi mwa wapiganaji wa Kiislam, na bunge linalotambuliwa kimataifa kwa sasa linaendesha vikao vyake katika mji ulioko pwani ya Tobruk mashariki mwa nchi hiyo
Marekani imekuwa ikiongoza washirika wa kimataifa kufanya mashambulio ya anga dhidi ya IS nchini Iraq na Syria katika miezi ya karibuni.