Tuesday, December 02, 2014

MKAZI wa Kijichi ajishindia nafasi ya kutembelea hifadhi ya wanyama ya Selous kupitia Ndovu Golden Experience


MKAZI wa Kijichi ajishindia nafasi ya kutembelea hifadhi ya wanyama ya Selous kupitia Ndovu Golden Experience
MKAZI wa Kijichi Jijini Dar es Salaam, Samson Marwa amejishindia nafasi ya kutembelea hifadhi ya wanyama ya Selous katika droo inayoendeshwa na bia ya Ndovu kupitia kampeini yake ya 'Ndovu Golden Experience'.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Ndovu Victoria Kimaro alisema, mshindi huyu ameibuka kidedea baada ya kuwagaragaza wenzake katika kampeini hiyo na kupata nafasi ya kwenda katika hiyo hifadhi na mtu mmoja.

Victoria alisema, lengo la kuanzisha kampeini hiyo, ni kuwapa fursa watanzania kujivunia rasilimali zao, hasa kumlinda mnyama Tembo ambaye anaibeba nembo ya bia hiyo.

"Naimani kuwa, washindi wayafarijika mno kutembelea hiyo mbuga kwani, watapata nafasi ya kuwaona wanyama wengi mno akiwemo Tembo, na pia sisi kama Ndovu tutawagharia washindi Malazi, Chakula pamoja na usafiri,"alisema. Aliongeza kwa kuwataka watanzania kuitumia nafasi hiyo, kabla ya droo hiyo kufikia tamati wiki ijayo, na washindi wanne kupatikana ambao wataambatana na wenzao wanne ambao kila mmoja atachagua.

Naye Inspekta wa kampuni ya Gaming Board of Tanzania, Humud Semvua ambao ndio wachezeshaji wa droo ya kuwapata washindi aliwapongeza watanzania kwa kuchangamkia fursa hiyo adimu kutokana na wageni wengi kutembelea hifadhi hizo.

"Watanzania wamejitokeza kwa wingi na kufungua chini ya kizibo, wiki iliyopita tulipompata mshindi watu 3754 walituma meseji na wiki hii ambayo tumempata Samson zaidi ya watanzania 4390 wametuma meseji, hivyo inaonyesha jinsi gani watanzania walivyoamka na kuthamini maliasili zao,"alisema.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya, AIM GROUP LIMITED, Emma Edward akichezesha droo ya tatu kupitia Bia ya Ndovu Special Malt wakati wa kumtangaza mshindi wa tatu atakayetembelea hifadhi ya wanyama ya Selous Dar es Salaam jana (kulia) ni Meneja wa Bia hiyo, Victoria Kimaro na (katikati) ni Ofisa wa Mwandamizi wa Bodi ya inayosimamia michezo ya kubahatisha, Humudi Semvua.
Meneja wa Bia ya Ndovu, Victoria Kimaro (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akimtangaza mshindi wa tatu katika droo ya tatu ya bia hiyo (kushoto) ni Ofisa Mwandamizi wa Bodi inayosimamia michezo ya kubahatisha, Humudi Semvua.