Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa leo amehudhuria maadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyoadhimishwa na Manispaa ya Ilala kwenye kata ya Vingunguti na ametumia fursa hiyo kuhamasisha wanaume kupima VVU kwani takwimu zinaonyesha asilimia ndogo ya wanaume wanajitokeza kupima.
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa akipatiwa maelezo kutoka kwa mmoja wa wataalamu wa maswala ya VVU wakati alipotembelea maadhimisho hayo.
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa akipatiwa ushauri nasaha kutoka kwa Daktari kabla ya kuamua kupima VVU.
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa akipima VVU.
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa akizungumza wakati akiwahamasisha vijana na watu mbali mbali kuwa na utamaduni wa kupima afya zao wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyoadhimishwa na Manispaa ya Ilala kwenye kata ya Vingunguti.