Kampuni ya Bima ya REAL Tanzania sasa imekuwa ni moja kati ya makampuni makubwa rasmi chini ya Kampuni ya Britam ambayo inatoa huduma mbalimbali za kifedha. Hii inafuatia kununuliwa wa Kampuni hiyo ya Bima na Kampuni ya Britam kutoka Kenya.
Kufutia hatua hiyo Kampuni ya REAL itakuwa na wigo mpana wa kutoa huduma za bima zikiwemo bima za Afya na Bima za maisha ambazo tayari kampuni ya Britam imekuwa ikitoa kwa muda mrefu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Muungano huu utaboresha huduma za bima nchini Tanzania na Afrika Mashariki ambayo kwa sasa Britam inanguvu ya kifedha, kiteknolojia na rasilimali watu.
Kufutia hatua hii, Britam sasa inaongoza kwa ukubwa wa kijografia kuliko Kampuni zoter za Bima Afrika Mashariki, pia Kampuni hiyo inashikilia nafasi ya pili kulingana na pato la ziada.
Mchakato wa ushirikiano na muungano wa Kampuni hizo mbili umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa sasa na kufuatiwa na kupata kibali kutoka kwa mdhibiti wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya nchini Kenya na kutekelezwa na washiriki kutoka Britam na REAL kwa kusaidiwa na Kampuni ya Usimamizi wa Kimataifa ya Mckinsey na washauri wengine.
"Kutokana na muungano wa Kampuni hizi mbili, uwepo wetu umekuwa kwa sehemu kubwa sana," alisema Bwana Peter Munga, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REAL na Britam Tanzania.
Bwana Munga aliendelea kusema kwamba muungano huo ni moja kati ya makampuni ya kutoa huduma za Bima katika Afrika Mashariki, kwani sasa Kampuni hizo zinatoa huduma katika nchi 7 tofauti ambazo ni; Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini, Malawi na Msumbiji.
Pia aliwahakikishia wamiliki wa hisa, wauzaji, watoa huduma za bima na wadau wengine kwamba wote wenye mikataba na Kampuni hizo mbili bado zitaendela kudumu hadi mwishoni mwa mwaka na kila Kampuni itawajibika kwa madeni yeyote wanaodaiwa kwa kipindi kilichobaki.
Kuungana kwa Kampuni hizo mbili ni fursa kwa Britam kuongeza uwepo wake katika soko la kitaifa na Afrika Mashariki na pia kuongoza soko katika biashara zote ambazo inazifanya.
Muungano wa Kampuni hizo mbili pia unaonekana kama hatua ya kwanza ya kuimarisha sekta ya Bima Tanzania ambayo ina ushindani mkubwa. Soko la Bima Tanzania lina zaidi ya makampuni 29 yanayofanya kazi katika soko hilo.
Muungano huu inaiwezesha Britam kutekeleza mkakati wake we kupanua biashara yake ya Bima na pia kutoa huduma zingine mbalimbali katika maeneo muhimu ya kijografia kama Tanzania ambayo yameonyesha uwezo mkubwa wa kukuwa kiuchumi barani Afrika.